WAZIRI BASHE AKUTANA NA BALOZI WA BELARUS
WAZIRI BASHE AKUTANA NA BALOZI WA BELARUS
Imewekwa: 11 Nov, 2024
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb), amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Belarus nchini Tanzania, Mhe. Pavel Vziatkin tarehe 22 Oktoba 2024 jijini Dodoma mwenye makazi yake jijini Nairobi, nchini Kenya.
Viongozi hao wamezungumza kuhusu kuimarisha ushirikiano katika kukuza Sekta ya Kilimo. Kwa mfano, Mhe. Balozi Vziatkin ameeleza kuwa Belarus imepiga hatua zaidi katika viwanda vya kuzalisha zana za kilimo na mbolea.
Waziri Bashe ameshukuru ugeni huo na kuonesha utayari wa Tanzania kushirikiana katika Sekta. Amesema Tanzania inakaribisha zaidi wawekezaji katika maeneo ya viwanda vya kuzalisha na kuunganisha zana za kilimo.
Aidha, Mhe. Balozi Vziatkin amemueleza Waziri Bashe kuwa Belarus ni miongoni mwa waagizaji wa mazao ya chai, kahawa, mbogamboga na matunda kutoka nchi mbalimbali zikiwemo nchi za Afrika Mashariki.
Viongozi hao wamefunga mazungumzo kwa kuonesha utayari wa majadiliano ya ununuzi wa mazao ya kilimo yakiwemo chai, kahawa na mbogamboga moja kwa moja kutoka Tanzania.