Dkt. Hussein M. Omar Naibu Katibu Mkuu (Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula)
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) akizungumza na Vyombo vya Habari jijini Dodoma, tarehe 17 Aprili 2025 kuhusu kupokea taarifa ya Serikali ya Malawi ya kuzuia kuingiza mazao ya kilimo nchini humo kutoka Tanzania yakiwemo Unga, Mchele, Tangawizi, Ndizi na Mahindi. Ameeleza msimamo wa Tanzania ni kuwa endapo Serikali ya Malawi na Afrika Kusini hazitabadilisha msimamo wao wa kuzuia mazao ya Tanzania kufikia tarehe 23 Aprili 2025, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo itazuia uingizwaji wa mazao na bidhaa zote za kilimo kutoka nchi hizo mbili, na hatua hizo zitaenda sambamba kutoruhusu bidhaa zinazopitia katika bandari na njia nyingine za usafirishaji (on transit cargo) hapa nchini kwenda Malawi na Afrika Kusini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli akizungumza katika uzinduzi wa Mafunzo ya Maafisa Ugani tarehe 17 Aprili 2025 katika Chuo cha Kilimo cha MATI Mlingano, Wilaya ya Muheza, Mkoani Tanga na kuwataka Maafisa hao kuendelea kutoa huduma na ushauri bora kwa wakulima ili kuwa na matokeo chanya.